top of page

Dini ya Kiislamu kuipiku ile ya Kikristo kwa ukubwa 2070

ile ya Wakristo ifikiapo 2070

Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa baada ya Ukristo kwa sasa lakini inakua kwa haraka sana.

Hata hivyo hilo huenda likabadilika iwapo mwenendo wa watu wanaojiunga na dini hiyo utaendelea, kulingana na utafiti uliochapishwa na kituo cha utafiti cha Marekani Pew Research Center.

Kulingana na utafiti huo Uislamu unakuwa kwa haraka ikilinganishwa na dini nyengine yoyote ile duniani.

Itaipiku dini ya Kikristo ifikiapo 2070 kulingana na makadirio yake na hivyobasi kuwa dini yenye ufuasi mkubwa duniani.

  • Umoja wa Wakristo na Waislamu Kibera

  • Mkahawa wakataa kuwahudumia wanawake Waislamu Ufaransa

  • Msikiti mkubwa Afrika wajengwa Algeria

Mwaka 2010 taifa la Indonesia ndilo taifa lililokuwa na idadi kubwa ya Waislamu duniani lakini sasa India huenda ikawa na wafuasi wengi zaidi duniani ifikiapo 2050. Hata hivyo taifa hilo litakuwa na wafuasi wengi wa dini ya Hindu. Idadi ya Wakristo nchini Uingereza na Ufaransa itashuka kwa asilimia 50 na asilimia 10 ya watu wanaoishi Ulaya wanakadiriwa kuwa Waislamu kufikia 2050.

Albright asema ''yuko tayari kuingia sajili ya Waislamu''

Wanne kati ya Wakristo 10 duniani watakuwa wakiishi katika jangwa la sahara barani Afrika.

Na nchini Marekani mmoja kati ya watu 50 watakuwa Waislamu kufikia 2050.


© 2017 SAUTI YA UPONYAJI. Proudly created with PASKAL LINDA.

bottom of page