top of page

Polisi Afrika Kusini wanaendelea kumtafuta mtoto aliyetoweka

Durban, Afrika Kusini.

Polisi nchini Afrika Kusini wanaendelea kumtafuta mtoto mmoja aliyetoweka, baada ya gari la familia yao kutekwa nyara katika eneo la Durban siku ya Ijumaa.Mtoto mwenye umri wa mwezi mmoja, Siwaphiwe Mbambo, alikuwa katika kiti cha nyuma cha gari la mamake, pale gari hilo lilipotekwa na wanaume wawili waliokuwa na silaha nje ya duka moja kubwa la kununua bidhaa.

Mamake alimnyakuwa mwanawe wa kiume wa miaka minane,

lakini majambazi hao walitoweka kwa kasi na gari hilo, huku mtoto huyo mchanga Siwaphiwe, akiwa ndani.Gari hilo lilipatikana baadaye na maafisa wa polisi bila ya mtoto huyo.Zaidi ya maafisa 100 wa polisi wamo katika msako mkali ya kumtafuta mtoto huyo, katika kampeini inayoendeshwa na vyombo vya habari ya mtoto kuibiwa nchini humo.

Watekaji nyara hao waliliendesha gari hilo kwa kasi, huku mtoto huyo mdogo akiwa bado ndani, maafisa wamesema.Gari jeupe aina ya Toyota Yaris, limepatikana, lakini mtoto huyo bado hajapatikana.

Msemaji wa polisi Thulani Zwane, amesema kuwa operesheni ya kumsaka mtoto huyo, inayohusisha maafisa wa polisio pamoja na kitengo cha mbwa wa kunusa, unaendelea hadi msichana huyo mdogo apatikane.

"Jukumu letu la kwanza ni kumpata mtoto huyo," Bw Zwane amesema.


© 2017 SAUTI YA UPONYAJI. Proudly created with PASKAL LINDA.

bottom of page